Pages

Saturday, May 9, 2015

MPYAA!!! NDOA YA MSANII WA SONGEA MOVIE MR & MRS SIDNEY MWAKAJIRA YAWA GUMZO NI UTATA MTUPU!! ONA KILICHO JILI SIKU YA NDOWA!

Katika maisha kuna sherehe kuu tatu nazo ni kuzaliwa, kufunga ndoa na kufa. Hizi siku kuu tatu nilazima kama binadamu uzipitie na uzipe kipaumbere.Ijuma, ‎February ‎27, ‎2015, ‏‎3:33:40 PM . Ni siku ambayo haitakaa isaulike ni siku ambayo kwa mala ya kwanza kutokea na haikuwai kutokea kabla. Kwa upande wa wasnii wa mkoa wa Ruvuma. Ilikua kama siku ya utakaso kwani nisiku ambayo Kwa mala ya kwanzan Wasanii wawili kutoka katika pande za Ngoni Land na maanisha Ruvuma ambapo mmoja akitokea kundi la TAANISI arts Group (SIDNEY MWAKAJIRA aka PEPE) na mwingine kutoka WZALENDO arts Group (NUSRATH aka VICK) waliunganika na kua mwili mmoja nikimaanisha kufunga ndoa au pingu za Maisha.
1

MR & MRS SIDNEY MWAKAJIRA PEMBENI NI WASINDIKIZAJI WAO
Walifikia uamuzi huo bila kuimizwa na mtu ni kwa mapenzi tu ya dhati na si kuchezeana kisha kupotezeana muda. Tukio hili lili wafungua baadhi ya wasanii masikio na kuhisi walichelewa kufanya maamuzi kama ya wawili hao na wengi wao wali ahidi kufanya kama Sidney. Siku hii ilikua ya furaha sana kwa wawili hao na wazazi wa pande mbili tofauti.

2

MRS. SIDNEY BI NUSURATH AKIWA NA MSIMAMIZI WAKE WAKIWASILI UKUMBINI.
 Mwandishi alipata bahati ya kuzungumza na Bbi Harusi naye alikua na haya ya kusema. "Nina furaha sana kwa siku yaleo maana ni ndoto ambayo nilikua naiota kila siku kuolewa na mwanaume ninaye mpenda kwa maisha yangu labda mungu atutenganishe. lakini pia kuolewa bahati Baba so namshukuru sana mungu kwa kunipa Mwanaume wa maisha yangu" Alimaliza kwa kusema hivyo huku akiwa  ana furaha sana!

3

MATHAYO MANASE MZALENDO & BWANA HARUSI
"Nimeamamua kuchukua uamuzi huu wa kufunga ndoa Kwasababu kuu tatu 1.Nampenda sana mke wangu na ndio maana naamua kuthibitiha hili 2.Naitaji kutulia na kuepuka michepuko maana magonjwa mengi siku hizi 3.Nimechoka kumdhini sasa nataka kuhalalisha mbele za Mungu mwenyezi aliye juu mbinguni." Alisikika Bwana Sidney Mwakajira alipo kua akihojiwa na Mwandishi wa Mzalendo Blogspot. Alionekana kuwa kama mtuasye amini kailicho tokea. 

4

MATRONI AKIMSAIDI BI HARUSI KUKATA KEKI

5

BIBI HARUSI AKIWA NA MATRONI WAKE
Ni siku ambayo ilikua na baraka na mungu kuonyesha alipokea ndoa yao akaiachia mvua.  Tuungane mimi na wewe kuwaombea wawili hawa waoate kudumu katika maisha ya ndoa yao kwakuwa wanakwenda kuanzamaisha yenye changamoto. Mungu awabariki nawawe na maisha marefu yenye maisha meme na yenye furaha!

NB:
Huu ni mwanzo wa kuinua sanaa ya mkoa wa Ruvuma na wasanii wake ungana nasi kusaport hizi arakati ili sanaa ifike mbali mpaka nje ya mipaka. By Mathayo Mzalendo



KAMA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE APO CHINI KWENYE SEHEMU WALIO ANDIKA COMMENTI








No comments:

Post a Comment