Pages

Wednesday, May 6, 2015

MASIKINI SENJERE!!!! AWAACHIA NENO ZITO WASANII WA MAIGIZO SONGE AKA SONGEA MOVIE!! WASIPO ZINGATIA WATAIUA TANSINIA YA FILAM SONGEA. KUJUA ZAID POFYA HAPA

Msanii maarufu nchini AHMADI YASSINI NIKOTWA maarufu kwa jina la SENJELE kutoka katika mikono salama ya WJ FILM PRODUCTI, kama utakua umetizama Moja kati ya filamu alizo wahi kushiliki auta pata tabu kummtambua na hizi nimiongoni mwa film alizo shiliki KIVULI, KIJACHO,MCHANGA NA KENI, nk. Msanii huyu gwiji katika nyanja za KOMEDY mzawa wa kusini mwa Tanzania katika himaya ya NGONI LAND aka RUVUMA Jana tarehe 6/5/2015 alifanya kikao na wasanii wa maigizo  ikiwa pamoja na kuwa shukuru kwa ushilikiano walio mpa katika kipindi kigumu cha kumsindikiza mama mzazi wa huyu msanii katika safari yake ya mwisho lakini pia kuwa aaga wasanii. Kikao kilifanyika katika kiwanja cha ZIMANIMOTO.


  1.  

     M/kiti wa CHAHAWAWARU  MOHAMED CAHAMA JAA AKA MR NGUNGUTA chama cha wasanii waigizaji ruvuma akifungua kikao na  kumkaribisha msanii SENJERWE azungumze machache.

Msanii AHMAD YASINI NIKOTWA AKA SENJERE akitowa ya moyoni.

Anaendrea kutoa yake hapa ni baada ya kutoa maneno yake mazito matatu na yene ujumbe mzito wakuumiza vichwa vya watu. Alisema ili uweze kuwa msanii mzuri ni lazima uzingatie herufi tatu nazo ni
  • A= Dharau
  • E= Heshima
  • U= Uaminifu 
Kama vinavyo jieleza hapo juu bila hivi vitu vitatu hakuna kitakacho fanyika katika ubora wake .


VERONIKA GAYO, DOGO H , CHIDY LL, MR. NGUNGUTA. Wsanii baadhi wakiwa makini kumsikiliza SENJERA
Anaendelea kwa kusema kuwa amesikia kua hakuna  ushilikiano wala umoja katika tansinia ya sanaa hapa mkoani hususani katika sanaa ya Maigizo. Akasema kua nilazima kuwe na upendo na upendo hauwezi kuja kama hauna uruma ndani yako. kwanza lazima uwe na huruma ndipo useme unupendo kwa na maana huruma ndo huleta upendo. baada ya kumaliza kuzungumza yake yote ikiwa pamoja na kuwa shukuru wasanii alii waruhusu wasanii watoe oja zao  ndipo wasanii wakaanza kutoa haja zao.
  1.  
 Msanii MATHAYO MANASE MZALENDO akito haja yake .
Mathayo alizungumzia zaidi kwenye Uzalendo kama desturi yake na akadai lazima wasanii wawe wazalendo kwa kupenda kazi za nyumbani na kusapatiana ikiwa pamoja na kuungisana kazi wasanii kwa wasanii. pia kasema  Usianze kumpenda Ray wada kabla haujampenda Mathayo wa songea. akamalizia kwa Kununua CD ya URIDHI WA AJABU ilio shootiwa mokoani humo chini ya Mchalo vidio productioni IKISHILIKIANA NA wAZALENDO ARTS GROUP pamoja na wasanii wa mkoa waRUVUMA.

2.
Msanii NURDINI ASED AKA HIBRA. akiwa ni msanii wa pili kuchangia hoja yeye alichangia kuhusu kufanya kazi yenye bajeti ya kutosha ili wasanii wafanye kaze kwa moyo napia alizungumzia swala zima la kumuandaa msanii kabla ya kazii na sio kumkurupusha tu.
3
Msanii JUDITH NTANGA AKA MRICHUI. 
Wanawake nao hawa kuwa nyuma juu ya swala zima la maendeleo ya kuua kwa sanaa ya mkoa wa Ruvuma. yeye alichania juu ya swala zima la ushilikiano  akasema kuwa unaweza ukawa una stori lakini hauna pesa ya kufanyia kazi lakini kuna mtu mwingine hana stori lakini ana pesa ya kufanyie kazi kwanini usimpe yule mwenye pesa ili mkashilkiana na mkafanya kitu kizuri klwa makubaliani. lakini akagusia na ubunifu wakuanzisha mchezo wa comedy ambao utarushwa katika kituo cha keba tv.
4
Msanii HAJI.
Huyu nae alizungumza mengi sana lakini kubwa kuliko yote alitoa mambo matatu ya kufatwa na msanii ili aweze kufikia mafanikio yake ya biashara ya sanaa kwa huduma ya watazamaji. na mabo hayo kama ifatavyo
  • Kazi : Akimaanisha unafanya sanaa ili ikufanyie nini kwenye maisha yako?
  • Statasi : Akiwa na maana ya utambulisho wa msanii anajitamulishaje ili jamii ikutambue
  • Muonekano : Msanii una muonekano gani ili kuifanya biashara yako?
5
Baadhi ya wasanii wakiwa katika usikivu wa hali ya juu.
6
Msanii MUHAMEDI FUNG FUNGA aka AMBUJE
Yeye alichangia juu ya swala zima la majungu na kupakaziana ubaya ikwa pamoja na lawamam zisizo na maana kwa wasani wenyewe.
7
Wasanii wakiwa katika pozi ya usikivu.
9
Msanii CHRISS aka MAJARO
alifunga hoja kwa kuchangia kwa kusema uwingi wa makundi sio ndio kutoka lakini pia sio lazima wote tuwe wasanii wengine wawe washabiki. pia aliacha kauli isemayo wakati mwingine mchawi wa sanaa ya mkoa waruvuma ni msanii mwenyewe. kisha kikao kika fungwa na wasanii wakapeana mikono kwa kumuaga SENJERE.

10
Baadhi ya wasanii wakisubili kikao kuanza
11
12
Mr Ngunguta, Dogo H, Senjere
14

Madam Mriam Chabwela, Mdam Juni
15

Mzalendo &  Senjer

NB;
huu ni mweanzo wa harakati za kuinua sanaa mkoa wa Ruvu. Uzalendo huanzi nyumbani tuungane kuinua sana ya mkoa wetu.  by Mathayo Mzalendo






















No comments:

Post a Comment