Pages

Wednesday, May 13, 2015

DOWLOAD NEW AUDIO MAX J FT SAMIR - KIDOGO (OFICIAL/TRACK MP4)

Tizama vijana wa mkoa wa Ruvuma walivyo na kipaji. Ni mala chache sana kuona msanii ana kubali uwezo wa chipikizi na hapa utaamini maneno yangu SAMIL KA KAA!

DOWNLOAD NEW AUDIO EDDY MC FT CAMMY BWAY _ MAMA (OFICIAL TRACK MP4)

Pakua wimbo mpya wa Eddy Mc ft Cammy Bway - Mama. ningoma ambayo imeibua hisia za dhati juu ya upendo wa mama. Ngon Land 4 Ever.

DAWNLOAD NEW AUDIO DK NER FT G LUCK - MISS RAPA (OFICIAL/AUDIO MP4)

Pakua wimbo mpya wa Dk ner ft G luck - Mss Rapa. Nibonge moja la ngoma linalo tikisa Pande izi pia katika vyombo vyo habari kwa kua No 1 katika Top Ten za Radio ya nyumbani.

DOWNLOAD NEW AUDIO FOBY ONE - HAFANANI NAO (OFICIAL AUDIO MP4)

Pakua wimbo mpya wa Foby O NE - Hafanani nao. msanii kutoka kusini mwa tanzania pande za Ngoni Land oaka Songea Town.

DOWNLOAD NEW AUDIO J BIZZO DESTNATION FT DK NER & ROBY SONGEA - NDIVYO ILIVY (OFISIAL AUDIO MP4)

DOWNLOAD NEW AUDIO NEW MAC FT BLLACK JR-MAGIC MAMA

Tuesday, May 12, 2015

HATARIIII!!!!!!! HEBU TIZAMA MAISHA HALISI YA STARIRIGI WA MOVIE YA MTATA WA KITAA AKA MR. NGUNGUTA!!! MHUUU!!

MTATA WA KITAA ni moja kati ya Film zilizo fanya vizuri hadi kufikia atua ya kuamsha ushindani katika swala zima la utoaji Filam.Hali hii ilipelekea kila mtu anataka atoe Film ili aonekane yupo juu zaidi ya mwenzake. Hapa namzungumzia gwiji la film mkoani Ruvuma aka Ngon Land Bwana MBARAKA CHAMA JAA aka MTATA aka CHAMA aka MR. NGUNGUTA. Jina lake limekua kwa kasi sana mara baada ya kuachia film yake ya kwanza katika kampuni ya Mchalo vidio Production. Film ambayo ilileta mapinduzi makubwa hapa mkoani hadi kufikia kila mtu kutaka kushoot na kutoa film
1

MTATA WA KITAA POSTAZ
Gwiji huyu ana takribani miaka kumi 10 ndani ya sanaa na ndomaana namwita Gwiji kwa kipindi hiki chote anahaki ya kufanya kanzi nzuri zaidi ya hii. Kuna Film nyingi ambazo amewai kushiliki nazi ni kama ifuatavyo
  1. Magic School
  2. Dangerouz Camp
  3. Zengwe Comedy
  4. Mtaat wa kitaa
  5. Urithi wa ajabu 

Hizi film zote kashiliki na kuzitendea haki na hasa katika film ya mtata wa kitaa ambayo adi imefanya watu wamuogope wakihisi kile alicho kiigiza ni chakweli na kina husu maisha yake. lakini kumbe ni tofauti na kilicho fanyika ni kazi ya uwasilishaji wa maisha harisi ya jamii kitaaramu jukwaani.

2
MTATA WA KITAA AKIWA OFISINI KWAKE

Ni wasanii wachache sana ambao wana jishughurisha na shughuri nyingine tofauti na sanaa. Nilipata tabu sana kupata MTATA, ilinigharimu miezi miwili kumpata na kufanya maojiano naaye na kwa baati nzuri tulifanyia mazungumzo ofisini kwake. kazi kubwa ya Mtata  akiwa nje ya sanaa ni Mchinjioni. Richa yakua anakipaji cha kuigiza na utangazi pia ni Mchinjaji muri wa Ng'ómbe.

3
MACHINJIONI AMBAKO MTATA HUFANYIA KAZ.

Naipenda sana sanaa na ninaamini sikumoja jamii itanielewa nakutambua kipaji changu. Namshukuru mungu kwa kua kazi yangu ya kwanza imepokelewa vizuri na mashabiki wangu na wasione kimya najaribu kutaka kufanya kitu tofauti ili wapate radha na kazinzuri kutoka kwa MTATA. Nataka nifanye kazi ambayo itakwenda kufunika habari ya Mtata Wa Kitaa. Mashabiki wangu wakae mkao wa kura maana nipo jikonii naandaa chakula cha Myoyo yao"Alimalia kusema hivyo Mtata mara baada mahojiano na alipo ulizwa mbona kimya muda mwingi umepita.

4
MTATA AKIWA KIBANDA CHA KUPATIA CHAKURA/MAMA NTILIE AKISUBILI MSOSI

5
MTATA AKIWA ANAKIMBIZA NG'MBE WA KUCHINJA.

6
DANGEROUS CAMP KASHILIKI MTATA

7
URITH WA AJABU MTATA KASHILIKI

8
ZENGWE COMEDY MATA KASHILIKI

Uzalendop huanza kwa kupenda vitu vya nyumbani. Wasanii wameamua kufanya kazi ya sanaa ili watengeneze ajira ambayo ita wapa kipato na wakaepukana na tabia hatarishi. Kazi kwako ewe mdau kuwasaport vijana wako.......!


NB:
Nia ni kuinua sanaa ya mokoa wa Ruvuma na wasanii wake na huu ni mwanzo wa harakati zake. tunahitaji kufika mbali kisanaa lakini saport kubwa tunaitoa kwako ewe mshabiki na mdau!

KAMA UNAPENDA KUSAPORT VYA NYUMBANI BASI TOA MCHANGO WAKO WA MAWAZO  KWA KUTUANDIKIA APO CHINI WALIPO ANDIKA "COMMENT"

Saturday, May 9, 2015

MPYAA!!! NDOA YA MSANII WA SONGEA MOVIE MR & MRS SIDNEY MWAKAJIRA YAWA GUMZO NI UTATA MTUPU!! ONA KILICHO JILI SIKU YA NDOWA!

Katika maisha kuna sherehe kuu tatu nazo ni kuzaliwa, kufunga ndoa na kufa. Hizi siku kuu tatu nilazima kama binadamu uzipitie na uzipe kipaumbere.Ijuma, ‎February ‎27, ‎2015, ‏‎3:33:40 PM . Ni siku ambayo haitakaa isaulike ni siku ambayo kwa mala ya kwanza kutokea na haikuwai kutokea kabla. Kwa upande wa wasnii wa mkoa wa Ruvuma. Ilikua kama siku ya utakaso kwani nisiku ambayo Kwa mala ya kwanzan Wasanii wawili kutoka katika pande za Ngoni Land na maanisha Ruvuma ambapo mmoja akitokea kundi la TAANISI arts Group (SIDNEY MWAKAJIRA aka PEPE) na mwingine kutoka WZALENDO arts Group (NUSRATH aka VICK) waliunganika na kua mwili mmoja nikimaanisha kufunga ndoa au pingu za Maisha.
1

MR & MRS SIDNEY MWAKAJIRA PEMBENI NI WASINDIKIZAJI WAO
Walifikia uamuzi huo bila kuimizwa na mtu ni kwa mapenzi tu ya dhati na si kuchezeana kisha kupotezeana muda. Tukio hili lili wafungua baadhi ya wasanii masikio na kuhisi walichelewa kufanya maamuzi kama ya wawili hao na wengi wao wali ahidi kufanya kama Sidney. Siku hii ilikua ya furaha sana kwa wawili hao na wazazi wa pande mbili tofauti.

2

MRS. SIDNEY BI NUSURATH AKIWA NA MSIMAMIZI WAKE WAKIWASILI UKUMBINI.
 Mwandishi alipata bahati ya kuzungumza na Bbi Harusi naye alikua na haya ya kusema. "Nina furaha sana kwa siku yaleo maana ni ndoto ambayo nilikua naiota kila siku kuolewa na mwanaume ninaye mpenda kwa maisha yangu labda mungu atutenganishe. lakini pia kuolewa bahati Baba so namshukuru sana mungu kwa kunipa Mwanaume wa maisha yangu" Alimaliza kwa kusema hivyo huku akiwa  ana furaha sana!

3

MATHAYO MANASE MZALENDO & BWANA HARUSI
"Nimeamamua kuchukua uamuzi huu wa kufunga ndoa Kwasababu kuu tatu 1.Nampenda sana mke wangu na ndio maana naamua kuthibitiha hili 2.Naitaji kutulia na kuepuka michepuko maana magonjwa mengi siku hizi 3.Nimechoka kumdhini sasa nataka kuhalalisha mbele za Mungu mwenyezi aliye juu mbinguni." Alisikika Bwana Sidney Mwakajira alipo kua akihojiwa na Mwandishi wa Mzalendo Blogspot. Alionekana kuwa kama mtuasye amini kailicho tokea. 

4

MATRONI AKIMSAIDI BI HARUSI KUKATA KEKI

5

BIBI HARUSI AKIWA NA MATRONI WAKE
Ni siku ambayo ilikua na baraka na mungu kuonyesha alipokea ndoa yao akaiachia mvua.  Tuungane mimi na wewe kuwaombea wawili hawa waoate kudumu katika maisha ya ndoa yao kwakuwa wanakwenda kuanzamaisha yenye changamoto. Mungu awabariki nawawe na maisha marefu yenye maisha meme na yenye furaha!

NB:
Huu ni mwanzo wa kuinua sanaa ya mkoa wa Ruvuma na wasanii wake ungana nasi kusaport hizi arakati ili sanaa ifike mbali mpaka nje ya mipaka. By Mathayo Mzalendo



KAMA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE APO CHINI KWENYE SEHEMU WALIO ANDIKA COMMENTI








Friday, May 8, 2015

KIMENUKA KUSINI!! FILAMU YA URITHI WA AJABU YA ZUA UTATA MKUBWA! WALIO IGIZWA WAJA JUU!! VERONICA HOFU TUPU!!!!!!

Mwanamke anaye kuja kasi katika Tansinia ya Film nchini akitokea pande za Ngon Land katika dimbwi la vipaji  hapa  nazungumzia Mkoani Ruvuma. Mwana mama huyu anaye julikana kwa jina la Veronica Gayo aka Veronica Mwana wa Gayo. Kwa sasa ameachia Filam yake inayo fahamika kwa jina la URITHI WA AJABU ni filamu inayo fanya vizuri mpaka sasa mkoani Ruvuma na kila anaye parta bahati ya kuitizama ana baki kinywa wazi kwa kuto amini uwezo ario uonyesha humo ndani.

1.
URITHI WA AJABU POSSTAZ
Kwa kile kilicho igizwa ndani kimekwenda kuakisi maisha ya watu fulani ambao wanaamini kati imani ya kishilikina hususani Uchawi. kwa habari za chini chini nikwamba wale walio hisi wameigizwa wao walianza kuinama na kuona sasa wamejulikani.
Hapa utaona jinsi wasanii wa Mkoa wa Ruvuma walivyo jipinda kuakikisha Ujumbe unafika swadacta kwa jamii husika.
2
VERONICA GAYO AKIWA NA CD ZA URITHI WA AJABU
"Kwa sasa nimeamua kujikita kwenye Tansinia ya Filamu watu wategemee vitu vizuri zaidi kutoka kwangu kwakua nina amini kuwa nina kipaji na nina mwamini Mwalimu wangu wasanaa anaye kuza kipaji changu Mathayo Mzalendo. Pia nimeona wanawake wengi wako nyuima kujikita katika huu upande lakini nina waambia mwaka huhu 50/50 na wanaume. namungu atanilinda"

3
HAMZA KASSIM AKA DOGO H & VERONICA GAYO

 4
MRIAMU CHABWELA & DYNES KADOPE WAKIMPA SAPOT MSANII MWENZAO KWA KUNUNUA COPY

5
NURDIN ASEDY NAYE ALIMMUNGISHA MSANII MWENZAKE CD

6


 7
MR NAYUNGI & VERONICA GAYO WAKIZUNGUSHA CD MTAANI.
Wangoni sasa tumeamua kutangaza kazi zetu wenyewe sasa ni nyumba kwa nyumba mpaka wajue.



NB:
Imefika hatua sasa wakazi wa Ruvuma  tuwe wazalendo kwa kununua kazi za nyumbani ili kutengeza hajira za watu walio kata tamaa. Huu ni mwanzo wa kuinua sanaa ya mkoa wa Ruvum.By Mathay Mzalendo

KAMA UNA MAONI NA USHAURI COMENT HAPO CHINI TAPHARI

Thursday, May 7, 2015

UTATA!!! KAMERA MANI ALIE SHOOT VIDEO YA ZENGWE NA MTATA WA KITAA AWAGUMZO MJINI BOFYA HAPA KUONA ALICHO KIFANYA!!!!

KAMERA MANI PAUL BONIFASE AKA SILENT KILLAR

 Unapo zungumzia makamera mani mjini Songea utapigwa kama huta mtaja PAUL BONIFASE aka SILENT KILLAR. Ni mmoja kati ya Makamera mani wanao fanya kazi nzuri katika Tansinia ya Film mkoani Ruvuma. Umaarufu wake umekuja mara baada ya  kushut filamu kazaa hapa mjini ikiwemo 1,Mtata wa kitaa 2,Zengwe 3,Urithi wa Ajabu. na hizi ni zile ambazo zimepata umaarufu na kuwa sokoni tukiachana na zile ambazo bado azija ingia sokoni.
Pia Camera mani mkubwa huyu licha yakua anakabiliwa na changamoto kuba ya vifaa. lakini amefanya vitu vikubwa vya kushangaza hata makamera mani wakubwa kuachwa midomo wazii. na hata kupata mialiko mbalimbali nje ya mji kama vile Mbeya, Njombe, Makambako, Dar-es-alaam na Iringa.


HIHI NI MOJA KATI YA KAZI ALIZO FANYA URITHI WA AJABU.

"Naipenda hii kazi na ndoto yangu sikumoja tanzania nzima ageuze macho na kutizma Mkoa wangu. Kwakua sikuzote mwanzo ni mgumu lakini nita kabiliana na changamoto ili kutimiza ndoto zangu namu ananiona." Hii ni kauli alio nipa wakati namuoji juu ya kazi anazo fanya mbazo ziko tofauti na mtazamo wake.
HII NAYO KAZI ILIYO TOKA MIKONONI MWAKE ZENGWE COMEDY

Anaamini kama akiwezeshwa ana weza kuamisha soko la movie dar kuja songea. lakini si peke yake bali wewe na mimi ndo tunao weza kumfikisha eneo frani la kubadili mtizamo.


NB;
Huu ni mwanzo wa kuinua sanaa ya mkoa wa Ruvuma ili sanaa ya Mkoa wa ruvma ikue inategemea sana Mawazo ya wasanii na wadau. Uzalendo una anzia kupenda kwanza cha nyumbani. by Mathayo Mzalendo


KMA UNAMAONI AU USHAURI TAFADHARI COMENTI HAPO CHINI

Wednesday, May 6, 2015

MASIKINI SENJERE!!!! AWAACHIA NENO ZITO WASANII WA MAIGIZO SONGE AKA SONGEA MOVIE!! WASIPO ZINGATIA WATAIUA TANSINIA YA FILAM SONGEA. KUJUA ZAID POFYA HAPA

Msanii maarufu nchini AHMADI YASSINI NIKOTWA maarufu kwa jina la SENJELE kutoka katika mikono salama ya WJ FILM PRODUCTI, kama utakua umetizama Moja kati ya filamu alizo wahi kushiliki auta pata tabu kummtambua na hizi nimiongoni mwa film alizo shiliki KIVULI, KIJACHO,MCHANGA NA KENI, nk. Msanii huyu gwiji katika nyanja za KOMEDY mzawa wa kusini mwa Tanzania katika himaya ya NGONI LAND aka RUVUMA Jana tarehe 6/5/2015 alifanya kikao na wasanii wa maigizo  ikiwa pamoja na kuwa shukuru kwa ushilikiano walio mpa katika kipindi kigumu cha kumsindikiza mama mzazi wa huyu msanii katika safari yake ya mwisho lakini pia kuwa aaga wasanii. Kikao kilifanyika katika kiwanja cha ZIMANIMOTO.


  1.  

     M/kiti wa CHAHAWAWARU  MOHAMED CAHAMA JAA AKA MR NGUNGUTA chama cha wasanii waigizaji ruvuma akifungua kikao na  kumkaribisha msanii SENJERWE azungumze machache.

Msanii AHMAD YASINI NIKOTWA AKA SENJERE akitowa ya moyoni.

Anaendrea kutoa yake hapa ni baada ya kutoa maneno yake mazito matatu na yene ujumbe mzito wakuumiza vichwa vya watu. Alisema ili uweze kuwa msanii mzuri ni lazima uzingatie herufi tatu nazo ni
  • A= Dharau
  • E= Heshima
  • U= Uaminifu 
Kama vinavyo jieleza hapo juu bila hivi vitu vitatu hakuna kitakacho fanyika katika ubora wake .


VERONIKA GAYO, DOGO H , CHIDY LL, MR. NGUNGUTA. Wsanii baadhi wakiwa makini kumsikiliza SENJERA
Anaendelea kwa kusema kuwa amesikia kua hakuna  ushilikiano wala umoja katika tansinia ya sanaa hapa mkoani hususani katika sanaa ya Maigizo. Akasema kua nilazima kuwe na upendo na upendo hauwezi kuja kama hauna uruma ndani yako. kwanza lazima uwe na huruma ndipo useme unupendo kwa na maana huruma ndo huleta upendo. baada ya kumaliza kuzungumza yake yote ikiwa pamoja na kuwa shukuru wasanii alii waruhusu wasanii watoe oja zao  ndipo wasanii wakaanza kutoa haja zao.
  1.  
 Msanii MATHAYO MANASE MZALENDO akito haja yake .
Mathayo alizungumzia zaidi kwenye Uzalendo kama desturi yake na akadai lazima wasanii wawe wazalendo kwa kupenda kazi za nyumbani na kusapatiana ikiwa pamoja na kuungisana kazi wasanii kwa wasanii. pia kasema  Usianze kumpenda Ray wada kabla haujampenda Mathayo wa songea. akamalizia kwa Kununua CD ya URIDHI WA AJABU ilio shootiwa mokoani humo chini ya Mchalo vidio productioni IKISHILIKIANA NA wAZALENDO ARTS GROUP pamoja na wasanii wa mkoa waRUVUMA.

2.
Msanii NURDINI ASED AKA HIBRA. akiwa ni msanii wa pili kuchangia hoja yeye alichangia kuhusu kufanya kazi yenye bajeti ya kutosha ili wasanii wafanye kaze kwa moyo napia alizungumzia swala zima la kumuandaa msanii kabla ya kazii na sio kumkurupusha tu.
3
Msanii JUDITH NTANGA AKA MRICHUI. 
Wanawake nao hawa kuwa nyuma juu ya swala zima la maendeleo ya kuua kwa sanaa ya mkoa wa Ruvuma. yeye alichania juu ya swala zima la ushilikiano  akasema kuwa unaweza ukawa una stori lakini hauna pesa ya kufanyia kazi lakini kuna mtu mwingine hana stori lakini ana pesa ya kufanyie kazi kwanini usimpe yule mwenye pesa ili mkashilkiana na mkafanya kitu kizuri klwa makubaliani. lakini akagusia na ubunifu wakuanzisha mchezo wa comedy ambao utarushwa katika kituo cha keba tv.
4
Msanii HAJI.
Huyu nae alizungumza mengi sana lakini kubwa kuliko yote alitoa mambo matatu ya kufatwa na msanii ili aweze kufikia mafanikio yake ya biashara ya sanaa kwa huduma ya watazamaji. na mabo hayo kama ifatavyo
  • Kazi : Akimaanisha unafanya sanaa ili ikufanyie nini kwenye maisha yako?
  • Statasi : Akiwa na maana ya utambulisho wa msanii anajitamulishaje ili jamii ikutambue
  • Muonekano : Msanii una muonekano gani ili kuifanya biashara yako?
5
Baadhi ya wasanii wakiwa katika usikivu wa hali ya juu.
6
Msanii MUHAMEDI FUNG FUNGA aka AMBUJE
Yeye alichangia juu ya swala zima la majungu na kupakaziana ubaya ikwa pamoja na lawamam zisizo na maana kwa wasani wenyewe.
7
Wasanii wakiwa katika pozi ya usikivu.
9
Msanii CHRISS aka MAJARO
alifunga hoja kwa kuchangia kwa kusema uwingi wa makundi sio ndio kutoka lakini pia sio lazima wote tuwe wasanii wengine wawe washabiki. pia aliacha kauli isemayo wakati mwingine mchawi wa sanaa ya mkoa waruvuma ni msanii mwenyewe. kisha kikao kika fungwa na wasanii wakapeana mikono kwa kumuaga SENJERE.

10
Baadhi ya wasanii wakisubili kikao kuanza
11
12
Mr Ngunguta, Dogo H, Senjere
14

Madam Mriam Chabwela, Mdam Juni
15

Mzalendo &  Senjer

NB;
huu ni mweanzo wa harakati za kuinua sanaa mkoa wa Ruvu. Uzalendo huanzi nyumbani tuungane kuinua sana ya mkoa wetu.  by Mathayo Mzalendo